KIFO CHA MBWA WAKE CHAMCHANGANYA KIUNGO ERIK LAMELA WA TOTTEN HAM

KIUNGO wa Tottenham Hotspur, Erik Lamela amesema ameshachanganyikiwa kufuatia kifo cha mbwa wake wakati akipatiwa matibabu.

Lamela ni majeruhi kwa muda mrefu sasa kutokana na kukabiliwa na maumivu ya paja na anapata matibabu nchini Italia.

Lamela alisema kuwa alipata taarifa za kifo cha mbwa wake ambaye anaitwa Simba wakati alipokwenda nchini Argentina kuhudhuria maziko ya kaka yake.


“Wakati najiandaa kuanza safari ya kurudi Ulaya ndipo zikaja taarifa za kifo cha mbwa wangu, Simba, nimechanganyikiwa kumpoteza mbwa wangu,” alisema Lamela kwa masikitiko.

No comments