KIMWANA WA CRISTIANO RONARDO GUMZO TUZO ZA FIFA

NYOTA kibao wa soka walifurika mjini Zurich kuelekea kwenye tuzo za The Best FIFA Football Awards ambazo Cristiano Ronaldo alitangazwa mwanasoka bora.

Wanasoka bora wa kisasa wanafahamika kwa kujali mitindo ya mavazi na baadhi yao walitinga na wake ama rafiki zao wa kike na kupita nao katika zulia la kijani.

Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alijitokeza hadharani na kwa mara ya kwanza na rafikiye wa kike mpya Georgina Rodriguez akifuatana na mtoto wa mwanasoka huyo, Cristiano Jr.

Kocha wake Zinedine Zidane pia alitinga katika tuzo hizo akiambatana na mkewe, Veronique.


Beki wa Juventus, Dani Alves alikuwa amevalia suruali ya kushika mwili na koti na pia alitinga katika hafla hiyo akiwa amefuatana na “bebi” wake.

No comments