MCHEZA Komedi maarufu, Mussa Kitale amesema kitakachofuata baada ya kutamba na swaga zake za Kiluguru akitumia jina la “Mkude Simba”, ni kuigiza kama Mpemba.

Akiongea na Saluti5, Kitale amesema kuwa itakuwa ni rahisi kwake kuigiza Kipemba kutokana na kwamba anazifahamu kwa asilimia kubwa tabia na sifa za watu wa kabila hilo.

“Unajua, Wapemba hawajatofautiana sana na Warugulu, hasa katika tabia ya kubishabisha mambo ambayo pengine hata hawayafahamu, huku wakijifanya wajuaji wakati kumbe hakuna kitu kabisa,” amesema Kitale.


Amesema, kama alivyofanikiwa kuwashika mashabiki wengi kwa kuigiza Teja na Mkude Simba, ana hakika atawakamata vilevile atakapojikita kucheza kama Mpemba.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac