KLOPP AANIKA MCHAWI WA SOKA LA LIVERPOOL KWA SIKU ZA KARIBUNI

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametaja sababu kubwa ya timu yake kuboronga katika siku za karibuni kuwa ni kutokana na upangaji mbovu wa timu hiyo.

Katika siku za karibuni wachambuzi wa soka wamedai kuwa staili ya uchezaji wa Liverpool ya kushambulia kwa kasi na nguvu ndio kumechosha wachezaji.

Liverpool ilitolewa na Southampton kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi Jumatano iliyopita.

Hali imekuwa tofauti na timu hiyo ilipoanza nusu ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa kishindo kiasi cha kupewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa England.


“Napenda kusema uamuzi wangu katika upangaji wa timu ndio chanzo cha kuboronga kwa Liverpool,” alifafanua Klopp.

No comments