KOCHA ANTONIO CONTE AMUUZA MICHY BATSHUAYI KWA MASHARTI

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kwamba mshambuliaji wake raia wa Ubelgiji, Michy Batshuayi anaweza kuondoka Stanford Bridge lakini kwa sharti moja tu.

Gazeti la The Daily Star limemkariri mwandishi wa habari wa Ubelgiji Kristof Terreur akisema kwamba nyota huyo anaweza kuondoka na kutimkia West Bromwich Albion au Swansea City kama kocha huyo raia wa Italia atatafuta mbadala wake.

Terreur ameandika katika mtandao wa Betway kwamba anadhani Conte ataugulia maumivu makali kama atamwachia mwanasoka huyo kuondoka akiwa hana mbadala wake.


“Kabla hajaja katika klabu hii kulikuwa na mfumo wa kutumia washambuliaji wawili. Anatakiwa kuangalia nini amefanya kwa Romelu Lukaku na Morata au sasa kwa Diego Costa,” ameandika.

No comments