KOCHA CARLO ANCELOTTI ATANGAZA JEURI BAYERN MUNICH

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kwamba kocha wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti ni jeuri, hebu kwanza msikie.

Kocha huyo, Ancelotti amesema kuwa angekuwa na wasiwasi kama angekwenda mapumziko ya majira ya baridi ya michuano ya Ligi ya Bundesliga kabla haijafikia katika kiwango chake.

Kauli ya kocha huyo imekuja ikiwa ni baada ya mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa kufungwa na timu za Atletico Madrid na Rostov kwa bao 1-0 katika michuano ya Ligi ya Bundelsliga na Borussia Dortmund, pia na sare ambayo haikutarajiwa dhidi ya timu ya Cologne na Hoffenheim ikiwa nyumbani, jambo ambalo limezua hali ya wasiwasi kuhusu mbio zao za kuwania ubingwa.

Hata hivyo baada ya kupata ushindi mfululizo ukiwemo wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao katika mbio za kuwania ubingwa RB Leipzig huku wakiwa hawana uhakika wa kutwaa ubingwa mwaka 2017 licha ya kuwa wapo juu kwa zaidi ya pointi tatu katika msimamo wa Ligi hiyo ya Bundesliga, Ancelotti anadai kwamba jambo la muhimu kwao ni kuongeza kiwango katika msimu huu kwa sasa.

“Bado tunahitaji kuongeza kiwango lakini bado tuna muda kwa hilo,” Ancelotti aliuambia mtandao wa TZ.

“Kama tusingekuwa katika ubora katika kipindi cha kwanza msimu huu tungejutia kwa hilo,” aliongeza kocha huyo.


Alisema kuwa wanachokitaka kwa sasa ni kushinda taji la michuano hiyo ya Bundesliga na kuweza kwenda mbali katika michuano ya Ligi ya mabingwa na kama wataishia nusu fainali itategemea na mabao mengi ambayo ataweza kuyadhibiti.

No comments