KOCHA HERVE RENARD AJIWEKEA NAFASI KUBWA YA KUANDIKA HISTORIA FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA

KOCHA Mfaransa, Herve Renard ana nafasi ya kuandika historia kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoanza wikiendi hii.

Renard ambaye anainoa Morocco akiibuka kuwa bingwa, basi ataweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji la Afrika mara tatu na mataifa tofauti.

Mfaransa huyo tayari ametwaa taji hilo mara mbili, mara ya kwanza akiwa na kikosi cha Zambia mwaka 2012 na mwaka 2015 wakati akiinoa Ivory Coast.

“Mimi sio mtabiri bali ni mshindani. Tumejiandaa kadri ya uwezo wetu na tumejiwekea malengo basi kama kushindwa kwetu itakuwa kutolewa robo fainali,” alisema Renard.  


Morocco ina kibarua kigumu kwani iko kundi moja na bingwa mtetezi Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Togo ambayo inafundishwa na bosi wake wa zamani, Claude Le Roy.

No comments