KOCHA MICHO ASEMA CHANGAMOTO ILIYOBAKI KWA UGANDA NI KUTAZAMA MAFANIKIO YA SIKU ZA USONI

KOCHA wa Uganda, Sredojevic Mirutn “Micho” anasema changamoto kwao ni kuangalia mafanikio ya siku za usoni baada ya kutolewa mapema kwenye fainali za mwaka huu za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Micho ambaye ni raia wa Serbia alisema Uganda sasa inatakiwa kuanza maandalizi mapema ili kufuzu kwa fainali za mwaka 2019.

Alisema haoni sababu ya kusikitika kwa timu yake kutolewa mapema kwani ilipangwa katika Kundi lililokuwa na timu zenye uzoefu za Ghana, Mali na Misri.


“Tunapaswa kutosikitika bali tujipange ili turudi tena katika michuano hii,” alisema Micho.

No comments