KOCHA RANIERI AMPIKU ZIDANE TUZO YA KOCHA BORA WA MWAKA FIFA

KOCHA wa Leicester City, Claudio Ranieri alimpiku Zinedine Zidane na kunyakua tuzo ya kocha bora ya mwaka ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA).

Ranieri alipata tuzo hiyo baada ya kuiongoza Leicester City ambayo sio miongoni mwa timu vigogo kutwaa taji la England.

Zidane ambaye anainoa Real Madrid alikamata nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilichukuliwa na kocha wa Ureno, Fernando Santos.

Ushindani ulikuwa mkali katika nafasi hiyo kwani Zidane aliiongoza Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Santos aliipa Ureno Kombe la Euro msimu uliopita.


“Nimefurahi sana kushinda tuzo hii, ni heshima kubwa kwangu,” alisema ranieri baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na gwiji wa soka, Diego Maradonna.

No comments