KOCHA TOTTENHAM ATAKA TIMU ZOTE 'ZIISHANGILIE' KLABU YAKE IKIUMANA NA CHELSEA


KOCHA wa Tottenham Spurs  Mauricio Pochettino anataka vilabu vyote vya Premier League viwe nyuma yake wakati klabu yake itakapoikabili Chelsea Jumatano usiku.

Mauricio Pochettino amesema mchezo huo dhidi ya Chelsea utakuwa mgumu sana lakini ni nafasi nzuri kwao ya kuwasimamisha na kupunguza pengo la pointi 10 kati yao.

"Najua Chelsea watakuwa kwenye presha kubwa kwasababu watacheza huku wakijua timu zote zinaiombea dua mbaya," alisema kocha huyo wa Spurs.


No comments