KOCHA WA IVORY COAST AWASHUSHUA WACHEZAJI WAKE… asema walicheza chini ya kiwango mechi dhidi ya Togo

KOCHA wa Ivory Coast, Michael Dussuyer amesema nyota wa kikosi chake walicheza chini ya kiwango kwenye mechi yao ya Togo.

Ivory Coast ilitoka suluhu na Togo Jumatatu kwenye mechi ya kwanza ya Kundi C ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Dussuyer alisema kuwa nyota wake walikosa mbinu za maarifa za kuipenya beki ya Togo.


“Togo walijipanga vizuri wakati wachezaji wao wakishindwa hata kupiga pasi tatu kwenye mchezo huo,” alisema Dussuyer.

No comments