KOCHA WA MISRI ASEMA WAMEJIANDAA KUWAPA FURAHA MASHABIKI WA NCHI YAO

KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hector Cuper amesema wamejiandaa kuwapa furaha mashabiki wa Misri kwenye mashindano ya Afrika mwaka huu.

Cuper ambaye ni raia wa Argentina alisema maandalizi yamekwenda vizuri na anajipanga kuondoa kasoro ndogondogo kwenye kikosi hicho.

Kocha huyo wa zamani wa Valencia na Inter Milan alisema alijifunza mengi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Tunisia wikiendi iliyopita.


“Ilikuwa mechi nzuri iliyojaa ufundi mwingi. Ila ninafurahi kupata ushindi na kasoro zilizojitokeza tutazirekebisha,” alisema Cuper akizungumzia timu yake kuifunga Tunisia bao 1-0.

No comments