KOCHA WA TIMU YA TAIFA MISRI ASEMA WAMEPANIA KUTINGA FAINALI MATAIFA YA AFRIKA

KOCHA wa timu ya taifa ya Misri, Hector Cuper amesema kuwa wamepania kutinga fainali kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Misri leo inakabiliana na Morocco kwenye mechi ya robo fainali ya mashindano hayo.

“Baada ya kuifunga Ghana kwenye mechi ya mwisho ya makundi, sasa tunataka kusonga mbele hadi fainali,” alisema Cuper ambaye ni raia wa Argentina.


Cuper alikiri kuwa mechi ya leo dhidi ya Morocco itakuwa ngumu lakini ana matumaini na kikosi chake kufanya vizuri.

No comments