KOCHA WA UGANDA ASEMA TIMU YAKE INAKABILIWA NA KAZI NGUMU

UGANDA imebaki na mengi ya kujiuliza baada ya kuchakazwa mabao 6-0 na Tunisia katika mechi ya kujipima nguvu kabla ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kocha wa Uganda, Sredojevic Milutin “Micho” alisema timu yake inakabiliwa na kazi ya kufanya marekebisho ya makosa waliyofanya kwenye mechi hiyo iliyochezwa mjini Tunis, Tunisia Jumatano iliyopita.

“Ukweli ni kuwa wachezaji wangu walishindwa kuwakabili Watunisia waliocheza kwa kasi na uelewano wa hali ya juu,” alisema Micho baada ya mchezo huo.

Hata hivyo, nyota wa Uganda, Hassan Waswa alisema kuwa walijitahidi kadri ya uwezo wao, lakini aliahidi watakaa chini na kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

Uganda ilionyesha udhaifu mkubwa katika kuzuia mipira ya kona, faulo na krosi kwenye mchezo huo.

Uganda imepangwa katika Kundi gumu la C na timu za Misri, Ghana na Mali kwenye fainali hizo.

No comments