KONGO WATAMBA KUJIAMINI KUTWAA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

KIUNGO wa Jamhuri wa Demokrasia ya Kongo (DRC), Youssouf Mulumbu amesema wanajiamini wanaweza kutwaa Kombe la Afrika.

Mulumbu alisema kitendo chao cha kuongoza Kundi gumu la C kinadhihirisha ubora wa kikosi chao.

Kongo inakabiliana na Ghana leo kwenye mechi ya robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.


“Tuna umoja katika kikosi, tuna ari ya hali ya juu, nadhani tuna nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa,” alisema Mulumbu.

No comments