LEICESTER CITY YATHIBITISHA JAMIE VARDY ATAENDELEA KUBAKI

STRAIKA wa mabingwa watetezi wa Ligi ya premier, Jamier Vardy hataweza kuondoka ndani ya viunga vya King Power.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho cha “The Fox” zinasema kuwa straika huyo ana mkataba unaomalizika mwishoni mwa mwaka 2020 hivyo hakuna klabu inayoweza kumnyakua kwa sasa.

Kukanusha kwa tetesi hizi kunafuatia taarifa za hivi karibuni zinazosema kwamba kuna klabu kadhaa zinazotaka kuvunja mkataba wa mpachika mabao huyo wa mabingwa hao watetezi.

Hata hivyo, licha ya uongozi kukanusha, Vardy mwenyewe ameungana katika kuukana uvumi huo kwa kuweka bayana ukweli ulivyo.

Akizungumzia uvumi huo, mchezaji huyo wa zamani waFleetwood Town alisema:

“Nina furaha kuona bado tunaendelea kupambana kwa ajili ya klabu. Sitarajii kuondoka katika kipindi ambacho nina mkataba wa zaidi ya miaka mitatu mbele.”

“Kwa ajili hii ninajivunia kuwa hapa kwa kipindi kirefu. Ninataka kuwa sehemu ya kupambana kwa ajili ya kulinda hadhi na heshima tuliojiwekea tangu msimu uliopita.”

“Leicester City ilionyesha haikuwa na madhara wakati nikiwasili hapa miaka mitatu. Ni vigumu kupima mafanikio haya kwa muda huu lakini inanifanya nione kuna jambo limefanywa nami nikiwa sehemu ya hayo yote.”


“Ninafarijika na uwekezaji huu wa klabu ambao umenifanya niwe mtu wa kuitumikia kwa nguvu zangu zote kama sehemu ya kulipa fadhila, hadhi na heshima kwa kufanya kazi maradufu,” amesisitiza Vardy.

No comments