LIVERPOOL WAENDELEA KUMPIGIA MAHESABU SERGIO RAMOS

MJOGOO wa jiji la London bado wanawaza kupata huduma ya nyota wa Real Madrid, Sergio Ramos ambaye wamekuwa wakimfukuzia tangu msimu uliopita.

Hata hivyo, klabu anayoichezea mlinzi huyo “katili” ya Real Madrid imekuwa ikikanusha mara kadhaa suala la kuondoka kwa Ramos ambaye pia ndiye nahodha wa kikosi cha mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ramos amekuwa akihusishwa na kujiunga na Liverpool katika usajili wa msimu uliopita ambapo pia alikuwa akihusishwa kutakiwa na Manchester United.

United wanatajwa katika dili la kumfukuzia nyota huyo wa Real Madrid kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mashetani wekundu hao.


Awali Liverpool waliweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya sergio Ramos kabla ya Madrid hawajaweka bayana kuwa dau la kiungo huyo ni mil 45 ingawa pia wamebainisha kwamba mlinzi huyo hauzwi kwa gharama yoyote.

No comments