LIVERPOOL YAHAHA KUPATA SAINI YA BEKI MATEO MUSACCHIO WA VILLAREAL

LIVERPOOL haitaki mchezo imeamua kufanya kweli kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha msimu ujao na safari hii inakwenda spidi kwa ajili ya kupata saini ya beki wa Villareal ya Hispania, Mateo Musacchio.

Raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 26, amekuwa katika rada za majogoo wa jiji la London tangu msimu wa usajili wa dirisha la mwezi Agosti, mwaka jana.

Ingawa vita za kumwania mlinzi huyo wa kati ni kubwa kutokana na kuwindwa pia na Manchester United, lakini Liverpool wameweka mezani ofa ya pauni mil 24.

Wakala wa mchezaji huyo amethibitisha kuwepo kwa mbio za klabu hizo mbili kwa mteja wake huyo lakini amebainisha kuwa Liverpool wana nafasi kubwa ya kushinda vita hiyo ya usajili.

Klabu yake ya sasa ya Villareal imekiri kupokea ofa kwa ajili ya Mateo Musacchio ambayo imefikia pauni mil 24 ya uhamisho, huku ofa binafsi za straika huyo ikiwa ni pauni mil 25.


Taarifa zaidi ndani ya Anfield zinasema kuwa klabu hiyo imeweka bayana azma yake ya kutaka kumpa mkataba wa miaka mitatu mlinzi huyo imara.

No comments