Habari

LIVERPOOL YASHINDWA KUTINGA FAINALI YA EFL CUP …YAPIGWA TENA 1-0 NA SOUTHAMPTON

on

Liverpool imeshindwa kutinga fainali ya EFL Cup baada ya kufungwa 1-0 na Southampton kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa Anfiled.
Bao pekee la  Southampton  lilifungwa na Shane Long kunako dakika za majeruhi na kuiacha hoi Liverpool iliyopanga kikosi chake kamili.
Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali baina ya timu hizo mbili uliochezwa Januari 11, Liverpool ilikubali kichapo kama hicho cha bao 1-0.
Southampton sasa itakumbana na mshindi kati ya Manchester United na Hull City ambazo zitachuana Alhamisi usiku huku United ikiwa na faida ya bao 2-0 ilizovuna katika mchezo wa kwanza.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *