MAJERUHI CRISTIANO RONALDO MGUU NDANI MGUU NJE COPA DEL REY

CRISTIANO Ronaldo na nyota wengine watatu wa Real Madrid wamefanya mazoezi peke yao juzi na kuashiria kuwa wako kwenye hatihati kucheza Kombe la Copa del Rey kutokana na kukabiliwa na maumivu.

Real Madrid inakabiliana leo na Celta Vigo kwenye mechi ya marudiano ya robo fainali ya Copa del Rey.

Mastaa wengine ambao hawakufanya mazoezi na wenzao ni pamoja na James Rodriguez na Danilo.

Ronaldo na wenzake wameongezeka katika orodha ya majeruhi wa timu hiyo. Majeruhi wengine wa Real Madrid ni pamoja na Marcelo, Luka, Modric, Gareth Bale, Pepe na David Carvajal.

No comments