MAJERUHI MUSONA APATA NAFUU NA KUIPA MATUMAINI ZIMBABWE

ZIMBABWE imepata moyo wa kufanya vizuri kufuatia habari za kupona kwa mshambuliaji wake tegemeo, Knowledge Musona.

Musona aliumia nyonga kwenye mechi ya kwanza ya Zimbabwe ambayo walifungana na 2-2 na Algeria ambapo alicheza dakika 12 tu.

Hata hivyo, staa huyo anayecheza soka nchini Ubelgiji alikosa mechi ya pili ambayo Zimbabwe ililala mabao 2-0 kwa Senegal.


“Musona anaendelea vizuri na ameanza mazoezi, bila shaka atakuwa fiti kwa mechi ya mwisho,” alisema daktari wa Zimbabwe, Nicholas Munyonga.

No comments