MANCHESTER CITY WAMPIGIA MAHESABU LUKAS BOEDER USAJILI WA KIANGAZI

MATAJIRI wa jiji la Manchester City wameweka jina la mlinzi wa Bayern Munich, Lukas Boeder katika orodha ya wachezaji wanaowania katika usajili wa majira ya kiangazi.

Tayari matajili hao wamepiga hodi katika klabu ya Leverkusen inayoshiriki Bundersliga.

Kwa mujibu wa Daily Mail, City inapambana na klabu nyinine zinazowania saini ya mlinzi huyo, zikiwemo klabu nyingi za Ulaya ikiwemo Barcelona.

Lakini City imetajwa kuwa katika mkakati mzuri wa kumnasa Boeder ikiwa ni hazina ya kukiimarisha kikosi cha msimu ujao.

Boeder amekuwa katika kiwango kizuri kwa miaka miwili iliyopita na kuwa tegemeo katika kikosi Bayer Leverkusen.


Mlinzi huyo amekuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kuingia katika rada za usajili wa Manchester City inayopanga kupambana kwa ajili ya mlinzi huyo.

No comments