MANCHESTER UNITED SASA YAWANIA SAINI YA KARIM BENZEMA

KLABU ya Manchester United imeonyesha haina masihara katika usajili wa kiangazi mwaka huu.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward sasa amekutana na wakala wa mchezaji Karim Benzema kwa ajili ya kuzungumza juu ya kuipata saini yake.

Hatua ya United ya kutaka kumsainisha Benzema mwenye umri wa miaka 27, ni kutaka kuimarisha zaidi safu ya ufumaniaji nyavu msimu ujao.

Mpango wa kumwania Karim Benzema unaratibiwa kwa karibu na bosi wa mashetani hao, Jose Mourinho ambaye pia anasaka saini za wachezaji mbalimbali kwa ajili ya usajili wa majira ya kiangazi.

Wakati ule Benzema alikubali kutua Real Madrid kwa dau la pauni mil 35 huku Alex Ferguson akimsainisha Michael kama mbadala wake.

Katika usajili wa dirisha la mwezi Agosti mwaka jana, Mourinho alipambana kwa ajili ya kuwanasa Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic.


Wachunguzi wa masuala ya soka wa kimataifa wanauchukulia usajili wa karim Benzema kama hatua ya klabu hiyo kutaka kuimarisha kikosi cha kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri katika duru la pili la premier ambayo kwa sasa inaongozwa na vinara wa Ligi hiyo, Chelsea inayonolewa na kocha Antonio Conte.

No comments