WAKATI Everton ikiwania kumsajili Morgan Schneiderlin huku kiungo wa Old Trafford  naye akitamani dili hilo likamilike haraka, Manchester United imesema mchezaji huyo hataondoka kwa dau chini ya pauni milioni 20.

Kocha wa Everton Ronald Koeman anapambana ili kumnasa nyota huyo wa Kifaransa huku klabu hiyo ikiwa imeshapeleka ofa moja ambayo inaaminika ni chini ya pauni milioni 20 ambayo haina mashiko kwa United.

United imesisitiza kuwa mchezaji huyo hataoondoka labda kwa ofa itakayokaribia dau la pauni milioni 24 walilolipa miezi 18 iliyopita wakati walipomnunua kutoka Sothampton.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac