MANCHESTER UNITED YAPEWA USHAURI WA BURE… yashauriwa kumsajili Danny Drinkwater

HUU ni ushauri tu ambao ni juu yao wenyewe wa Manchester United kuukubali ama kuupotezea.

Katika kile kinachoaminika kutaka kuiona United ikirejea katika kiwango chake cha zamani, mashetani wekundu wameshauriwa kumsajili kiungo wa Lecester City, Danny Drinkwater.

Ushahuri huu umetolewa na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Manchester United, Rene Meulensteen.

Kiungo huyo wa mabingwa na premier msimu huuu Leicester City amewahi kupita Old Trafford kama mchezji kinda ambaye kwa sasa ni kati ya wachezaji wanaoweza kuirejesha katika uimara United katika msimu ujao.

Alisema kocha huyo kuwa United wamekosa wachezaji wa aina ya Drinkwater ambao wakipatikana watairudisha timu katika mazingira ya kuwa tishio kama ilivyo katika enzi ya kocha Alex Ferguson.

“Kama ukitaka kuichambua Leicester City na sababu iliyochangia kutwaa ubingwa huwezi kukosa kutaja kuimarika kwa idara yao ya kiungo ilivyoongozwa vyema na Drinkwater.”


Kiungo huyo mwenye miak 26 ni zao la United kwani ametokana na mradi wa kulea na kukuza vipaji ndani ya Old Trafford lakini alishindwa kupata mafanikio na kuamua kutimkia Leicester City mnamo January 2012.

No comments