MARADONNA AMPONDA RONALDO "KIAINA".. awabeza wanaodai bado yuko kwenye ubora wake

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama kasema wanaosema straika wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo yuko katika ubora wake kwa sasa ni waongo, straika wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradonna amesema kuwa anavyoamini kinara huyo hayuko katika ubora huo na huku akiitakia kila la heri klabu yake ya zamani ya Napoli katika mchezo wao wa Ligi ya mabingwa hatua ya 16 Bora dhidi ya Real Madrid.

Mwaka huu nyota huyo wa timu ya taifa ya Ureno umekuwa mzuri sana kwake baada ya kuiwezesha timu yake kutwaa taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa, taji la fainali za Mataifa ya Ulaya akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno “Euro 2016” na huku akinyakua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia “Ballon d’Or” kwa mara ya nne.

Mbali na hilo, pia katika kuonekana kwa mara ya mwisho katika kalenda ya michuano ya mwaka huu, ikashuhudiwa akitupia hat trick katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa klabu.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, Maradonna anaamini mchezaji huyo mwenye mabao 23 katika michezo 22 kwa nchi yake na klabu msimu huu hafanyi vizuri kulingana na uwezo wake.

Huku akiitakia Napoli kila la heri katika michuano ya seria A na huku ikienda kukabiliana na Ronaldo na Real katika hatua hiyo, anasema kuwa staa huyo anaweza kuwa amerejea katika ubora wake wakati timu hizo zitakapokutana mwakani.

“Ningependa Real Madrid na Napoli zicheze leo kwasababu Ronaldo hayuko kwenye ubora wake,” alisema mkongwe huyo.


“Lakini kwa mwezi Februari anaweza kuwa katika ubora wa hali ya juu,” aliongeza. 

No comments