MASTAA WA ARSENAL WABEZA BAO LA “SCORPION” LA OLIVIER GIROUD

NYOTA wa Arsenal wamemwambia Olivier Giroud kuwa bao lake la scorpion “sio kali” ukilinganisha na lile lililofungwa na kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan.

Giroud alifunga bao kali kwa kisigino kwa staili maarufu kwa jina la scorpion kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.

Alifunga bao hilo baada ya Mkhitaryan kuwa amepachika bao la aina hiyo kwenye mechi dhidi ya Swansea City.


“Wakati tukiwa mazoezini wachezaji wenzangu wa Arsenal wamekuwa wakinizodoa kuwa bao la Mkhitaryan ndio kali zaidi,” alisema Giroud.

No comments