MATONYA AMVULIA KOFIA GIGY MONEY... asema ana sifa zote za kumfanya ashiriki kwenye video za wasanii mbalimbali

MSANII mkongwe wa Bongofleva, Matonya amemsifia “video vixen” Gigy Money kuwa ana sifa zote za kumfanya ashiriki kwenye video za wasanii mbalimbali nchini.

“Kwanza anajiamini, ni mbunifu na ana kila kitu ambacho kinafaa kwenye kazi ya muziki ndio maana na mimi nimemshirikisha kwenye video ya wimbo wangu wa “Hakijaeleweka”,” alisema Matonya.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Seif Shaaban, alisema kuwa video ya wimbo wake huo imetoka mwanzoni mwa wiki hii na imeshapata watazamaji wengi ambao wamekuwa wakiifuatilia.


Amesema kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimsema vibaya Gigy Money, lakini kwake (Matonya), anamuona kama ni mtu muhimu na mwenye kipaji cha hali ya juu.

No comments