MATS HUMMELS AKANA KUTAKA KUSEPA BAYERN MUNICH... asema bado yupoyupo sana tu

MLINZI wa wa timu ya Bayern Munich, Mats Hummels amezisikia taarifa za kutaka kuondoka na sasa amekanusha akisema bado yupoyupo kwanza Bundesliga.

Hummels anayeitumikia pia timu ya taifa ya Ujerumani mkataba wake unafika tamati majira ya mwaka 2021 ndani ya kikosi cha mabingwa hao watetezi.

Hatua hiyo inazufanya klabu mbalimbali za Ulaya Kutaka kupata saini yake na klabu za Arsenal na Manchester United na Real Madrid kugonga mwamba.

Mlinzi huyo aliyeng’ara kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil amesema kwa sasa anataka kutuliza akili yake akiwa na Munich.

“Uvumi wote huu ni jambo lingine ambalo sijaliweka katika vipaumbele vyangu, nitaendelea kuvumilia kusikia haya,” alisema Mats.


Bosi wa Manchester United Jose Mourinho alihitaji huduma ya mlinzi huyu kwa ajili kuimarisha kikosi chake kinachopambana kwa ajili ya kurejesha hadhi na heshima ya klabu inayopigania kushika nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu ya England msimu.

No comments