MCHEZAJI WA HULL CITY ALIYEVUNJIKA FUVU LA KICHWA AANZA KUONGEA

KLABU ya soka ya Hull City imesema nyota wake, Ryan Mason aliyevunjika fuvu la kichwa chake kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea ameanza kuzungumza baada ya kufanyiwa operesheni.

Hull City ilisema kuwa nahodha wa timu hiyo, Michael Diawsonm, daktari wa klabu, Mark Waller, Ofisa Tabibu, Rob Price na Katibu wa klabu, Mattwild walimtembelea juzi kwenye hospitali ya St. Mary, jijini London ambako amelazwa.

“Nahodha na viongozi wa klabu walimtembelea Ryan na aliweza kuzungumza angalau japo kwa shida. Alikuwa na kumbukumbu nzuri ya tatizo lililomkuta. Anaendelea vizuri baada ya operasheni,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Mason aligongana na beki wa Chelsea, Gary Cahirr wakati wakiwania mpira wa juu kwenye mechi baina ya timu hizo mbili wikiendi iliyopita.


Cahirr aliongozana na john Terry na kocha msaidizi wa Chelsea, Stive Holland kwenda kumwona mason hospitalini ambako amelazwa.

No comments