MECHI YA SENEGAL NA CAMEROON YAVUTA HISIA ZA MASHABIKI WENGI AFRIKA

KINYANG’ANYIRO cha michuano ya Kome la Mataifa ya Afrika (AFCON) kimefikia patamu baada ya kuingia hatua ya robo fainali.

Hata hivyo mchezo utakaopingwa Jumamosi kati ya timu ya Taifa ya Senegal “The Teranga Lions’, dhidi ya Camoroon umevuta hisia za watu wengi.

Timu hizo zote kutoka Afrika Magharibi zimeteka hisia za watu wengi kutokana na upinzani unaojitokeza kila zinapokutana timu hizo.


Ingawa mwaka huu Senegal wanaonekana wapo vizuri lakini kwa mechi kama hizo chochote chaweza kutokea. Cameroon wanaweza kusawazisha makosa yao ya mwanzo na kufanya makubwa.

No comments