MIHELA YA WACHINA YAZIDI KUZITETEMESHA KLABU ZA ULAYA NA MAKOCHA WAKE

KLABU za Ligi Kuu China zinaendelea kulitia kasheshe soko la wanandinga Ulaya na kwingineko kwa kumwaga fedha ya kutosha kuwanasa wachezaji wa daraja la kwanza kwa ubora, hasa wale wa kutoka Ulaya.

Straika wa zamani wa Man United na Man City, Carlos Tevez ni miongoni mwa wanasoka bora kabisa hivi karibuni kutimkia China na kuvuta mkwanja.

Hakuna shaka fedha hizo za China zimeanza kuwatisha makocha Ulaya kama ambavyo kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alivyowahi kusema: “Sielewi kwanini wanasoka wanakimbilia China.”

Kocha Antonio Conte nae ameibuka na kudai kuwa kocha aliyopewa supastaa wa Real Madrid, Christiano Ronaldo ili aende kucheza soka China sio sahihi.  

Klabu moja ya China imekubali kutoa pauni mil 250 ili aachane na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid na kwenda kucheza China.

“Nadhani sio sahihi kutumia fedha nyingi kuwarubuni wachezaji wakubwa. Sikubaliani na utaratibu huu,” alisema Conte.

Wakati na makocha wengine wakihofia fedha za China, tayari mchezaji wake mmoja Conte, Oscar ametimkia China kwa uhamisho wa pauni mil 60.


“Inawezekana kuwa hii ni hadithi tu, sitaki kuamini tunazungumzia suala la fedha, hapa mimi siamini lakini kama kuna ofa za aina hii basi hakuna mchezaji anayeweza kukataa.”

No comments