MIKE “IRON” TYSON KUMFUNDISHA CHRIS BROWN MBINU ZA KUMNG'ATA SIKIO SOULJA BOY

BIFU la Chris Brown na Soulja Boy limeonekana kuchukua sura mpya baada ya kubainishwa kuwa mwimbaji huyo wa kibao cha “Loyal” atapewa mazoezi na Mike Tyson ya namna ya kumtoa kwa KO rapa huyo mwenye umri wa miaka 26.

Katika video iliyopostiwa Jumapili usiku, bondia huyo bingwa wa dunia wa zamani ameahidi kumfundisha Brown na kumpa kila mbinu “chafu” iliyopo mchezoni.

“Hivyo imethibitishwa,” Tyson alisema katika video hiyo aliyoiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Nitamfundisha Chris, amenichagua kuwa mwalimu wake kwa ajili ya kumkabili Soulja Boy. Na Soulja Boy unazungumza ujinga gani? Nitamfundisha namna ya kumuuma mtu sikio. Ndio. Iko hivyo. Nitamfundisha kila mbinu chafu kumpiga kwa KO. Sitamfundisha kukimbia pambano.”

Alhamisi Soulja aliposti picha akiwa na bondia Floyd Mayweather na kuandika “Bingwa yuko na hii.” Kisha baada ya posti ya Tyson akaandika tena.

“Tyson utamfundisha Chris Brown kung’ata sikio? B**** Money Team haijawahi kupoteza pambano. Heshima kwako Floyd.”

Ugomvi baina ya wawili hao ulianza baada ya Soulja kusema wiki iliyopita kuwa alipoposti picha ya Karrueche Tran, brown alimpigia simu na kumtisha.


Soulja amechochea bifu akisema amewaalika Rihanna na Karrueche kwenye pambano lake na Chris Brown.

No comments