MISRI YASABABISHA CAF KUTAKIWA KUANGALIA UPYA KANUNI ZAKE

KUTOKANA na kubakiwa na kipa mmoja, Essam El Hadary mwenye miaka 39 kwenye michuano ya Afrika inayoendelea nchini Gabon, baada ya makipa wake wengine wawili kuumia misuli, imesababisha CAF kutakiwa kuangalia kanuni.

Makipa Ahmed El Shenawy na Sherif Ekramy wameumia na hawataweza kushiriki tena michuano ya mwaka huu ya AFCON na sasa wadau wa soka wanataka timu ziongezewe idadi ya wachezaji ama kuwe na nafasi tatu zinazoweza kujazwa wakati wowote.

Kutokana na kanuni za sasa, kila timu inapasa kuwa na wachezaji 23 pekee wanaoshiriki michuano hiyo ambapo timu nyingine zimekuwa zikiteua makipa watatu lakini inaonekana idadi hiyo ni ndogo baada ya janga lililowakuta Misri.


Kanuni za sasa za CAF zinasema hakuna timu inayoweza kuruhusiwa kuita mchezaji mwingine saa 24 kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

No comments