MIZENGWE YAANZA CHINA JUU YA WACHEZAJI KUTOKA LIGI ZA NJE

CHAMA cha soka nchini China kimesema kuwa pamoja na matumizi makubwa ya fedha kwa wachezaji wanaotoka katika Ligi mbalimbali lakini kuna kanuni ambazo lazima ziheshimiwe.

Chama hicho kimesema kwamba usajili unaofanywa unawavutia wengi na kupeleka majina makubwa lakini huko kuna kanuni zake na hawawezi kucheza wote kwa wakati mmoja.

Matumizi makubwa ya fedha katika soka lao yameleta majina makubwa katika mpira wao.

Si ajabu kuona majina ya Manuel Pellegrini, Andre Virras, Boas na wachezaji kama Gervinho, Hulk, Asamoah, Gyan wakiwa Ligi hiyo.

Carlos Tevez ameenda China na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani akilipwa pauni 615,000 kwa wiki katika timu ya Dhanghai Dhenhua, huku pia Oscar akiikacha Chelsea na kwenda Shanghai SIPG.

Bado pia klabu za China zinazidi kuhusishwa na usajili wa wachezaji wakubwa, wiki hii wakitajwa kuwa katika mbio za kumpeleka Costa katika Ligi yao.

Utitiri huu wa wachezaji wanaoingia China umewafanya wachezaji wanaotoka China kushuka thamani.


Lakini ili kulinda soka lao, Wachina nao wameamua kuweka sheria inayozibana klabu za nchini mwao kuhusu wachezaji kutoka nje.

No comments