MKONGWE RASHID PEMBE ATOA NENO KUHUSU VIJANA JAZZ ILIYOPOTEZA MSISIMKO

MPULIZAJI gwiji wa Saxaphone, Rashid Pembe “Profesor” amekiri kupungua makali kwa bendi yake ya zamani ya Vijana Jazz na kusema inaweza kurudi kwenye chati iwapo viongozi wake wa sasa watakubali mabadiliko.

Akiongea na Saluti5, Pembe ambaye sasa anamiliki bendi yake mwenyewe ya Mark Band, amesema enzi za utawala wake, baada ya kifo cha Chiriku Hemedi Maneti, ilibidi akubali kuiongezea nguvu bendi hiyo kwa kuwaleta waimbaji wanne wenye uwezo zaidi yao.

“Ilibidi nikubali mabadiliko kwa kuwang’oa kwenye bendi zao Benno Villa Antony, Jerry Nashon Dudumizi, Rahma Shari, Suleiman Mbwembwe na kuwaleta Pambamoto,” amesema.

Amesema ingawa pia viongozi wa ngazi za juu wanahusika katika kuirudisha bendi hii katika ubora wake, lakini lazima kwanza wanamuziki wenyewe wakubali kuwaleta wasanii wenye mbinu za kimuziki zaidi yao.  

No comments