MOURINHO AMPA BIG UP FELLAINI KWA KUWAPOTEZEA MASHABIKI WALIOKUWA WAKIMZOMEA

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amempongeza kiungo wake Marouane Fellaini kwa kuwapuuza mashabiki waliokuwa wakimzomea na kuacha soka lake “liongee”.

Fellaini amekuwa na wakati mgumu tangu asababishe penati iliyochangia Everton kusawazisha bao wakati walipofungana bao 1-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

“Nimefurahi kuona mashabiki wameacha kumzomea baada ya kuona jinsi anavyojitolea kwa ajili ya timu,” alisema Mourinho.


Mourinho alimsifia Fellaini kwa kueleza kuwa amekuwa na mchango mkubwa katika timu katika siku za karibuni.

No comments