MOURINHO AMWOMBA ROONEY KUIBEBA MANCHESTER UNITED KWA HALI NA MALI

JOSE Mourinho amemtaka mvunja rekodi ya ufungaji, Wayne Rooney kuisaidia Manchester United kutatua tatizo la kutopata ushindi wakati walipojitutumua na kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Stoke City Jumamosi na kuondoka na pointi moja.

Bao la kujifunga la Juan Mata liliwapa uongoze Stoke kuanzia dakika ya 19 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Britannia kabla ya Rooney kuiokoa kwa kusawazisha goli na kuipa pointi moja na bao hilo kumwezesha kuweka rekodi ya mfungaji wote wa United akifikisha mabao 250 na kuivunja ile iliyowekwa na Bobby Chariton.

Sare hiyo imemfanya Mourinho kutoshinda mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool.

Sasa baada ya Rooney kuisawazishia man United bao hilo Mourinho amemtaka kuisaidia timu hiyo kuondokana na jinamizi la kutoshinda kwenye mechi zake na hivyo kutaka awasaidie kupata ushindi kwenye kila mchezo.

“Ni mafanikio ya kushangaza na kufurahisha, lakini rekodi hiyo inamfanya rooney kuwa mchezaji wa kawaida na kuendelea kufunga mabao zaidi kwenye timu yetu,” amesema Mourinho wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Lilikuwa bao muhimu zaidi kwetu na katika timu ambayo ilishapoteza matumaini ya kupata pointi moja kwenye mchezo ule.”

Mourinho aliendelea kusema kwamba: “Hakika kwenye Ligi Kuu leo unawea kuona umetoka tena sare, kuna jambo la muhimu la kulifanya.”

“Timu pinzani ilifunga bila kutengeneza nafasi yoyote ya kufunga lakini sisi tulicheza kwa kutawala mchezo wote na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwani tulitengeneza sita hadi saba, lakini ilikuwa kazi ngumu kwetu.”

No comments