MOURINHO: KUSUASUA KWA MAN UNITED KUMELETA UMOJA NA UELEWANO KIKOSINI

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kuboronga kwa timu hiyo mwanzoni mwa msimu kumesaidia kuleta umoja na uelewano katika kikosi chake.

Mourinho alisema, katika kipindi ambacho timu yake inasuasua ilisaidia kuongeza upendo kati yake na nyota wa kikosi hicho.

“Kwa kawaida upendo katika timu huongezeka pale mnaposhinda, hata hivyo kwa Manchester United imekuwa kinyume chake kwani kipindi tunafanya vibaya ndio tuliweza kuongeza ukarimu katika kikosi,” alisema Mourinho.

Mourinho alisema wachezaji walitulia na kuendelea kumheshimu licha ya timu kuboronga.


“Sasa tunafaidi matunda kwa kushinda mechi mfululizo kwa sasa,” alisema Mourionho ambaye timu yake ilicheza na Reading juzi kwenye mechi ya mtoano ya kuwania Kombe la FA.

No comments