MWAMUZI MARK CLATTENBURG ASEMA ALIPOTEA NJIA YA KWAO BAADA YA "KUMTIBUA" MOURINHO KWA KADI NYEKUNDU

MWAMUZI wa Ligi Kuu England, Mark Clattenburg ametoboa siri kuwa alipotea nyumbani baada ya kukorofishana na kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.  

Clattenburg alimtoa nje ya uwanja Mourinho kwa kitendo chake cha kumpinga kwa kumuonyesha kadi nyekundu Ander Herrera.

Mwamuzi huyo alidai kuwa alikuwa mwenye mawazo mengi baada ya mchezo kiasi cha kujikuta amepotea njia wakati akiendesha gari akitokea Manchester kwenda katika mji wa Newcastle anakoishi.


“Nilikuwa natafakari uamuzi wangu nadni na nje ya uwanja. Niligundua kuna makosa niliyafanya. Ila ieleweke wazi kazi hii ni ngumu,” alisema Clattenburg kwenye mahojiano na shirika la habari la Associated Press.

No comments