MAMA MKANYE MWANAO YA AZAM FC YAPELEKA KILIO MSIMBAZI …Simba yaishia kunawa Mapinduzi Cup


SIMBA wamenawa lakini wameshindwa kula. Ndivyo unavyoweza kusema baada wakali hao wa Msimbazi kulambwa 1-0 na Azam FC kwenye fainali ya Mapinduzi Cup.

Kombora la nje ya 18 kutoka kwa kiungo wa Azam Hamid Mao lilitosha kabisa kupeleka kombe Chamanzi.

Katika mchezo huo uliopigwa Ijumaa usiku kwenye uwanja wa Amani, dakika ya 12 Hamid Mao akapokea pasi kutoka kwa Salum Abubakar na kumtazama kipa Daniel Agyei kabla ya kuachia shuti la ‘Mama mkanye mwanao’ lililokwenda moja kwa moja wavuni.

No comments