NEYMAR AWAPIKU RONALDO, MESSI KWA MKWANJA NJE YA UWANJA

NEYMAR ameongezwa mkataba katika dili lake la kuwa balozi wa brand ya miwani iitwayo “Polici” ya Italia akiingia katika mwaka wake wan ne kufanya kazi na kampuni hiyo.

Nyota wa Barcelona alitumia sehemu ya mapumziko yake ya wiki tatu baada ya La Liga kusimama kipindi cha Krismasi kwenda kupiga picha maalum ya uwanamitindo ya kutangaza brand hiyo ya miwani ya “Polici 2017.”

Alishirikiana na mwanamitindo mwanadada katika pozi mbalimbali za picha hizo sambamba na video zizizorekodiwa kwa ajili ya matangazo ya aina mbalimbali ya miwani hiyo.

Katika kuitangaza miwani hiyo, Neymar amefuata nyayo za David Beckham pamoja na nyota wa Hollywood, Bruce Willis, George Cllniy na Antonio Babdiras wakati alipokula shavu la kuwa balozi wa miwani hiyo 2013.

Kiujumla Neymar, 24, ni kati ya wachezaji wachache katika dunia ya soka ambao wanaingiza pesa nyingi nje ya uwanja kuliko uwanjani.


Jarida la Forbas liliripoti kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2016, asilimia 61 (pauni mil 30.5) ya mapato ya Neymar yaliyotokana na mikataba ya udhamini nje ya uwanja, kiasi ambacho ni takriban mara mbili ya asilimia 36 za dili za nje ya uwanja alizopata Cristiano Ronaldo, huku Lionel Messi akiingiza asilimia 34 ya kipato chake nje ya uwanja.

No comments