Habari

“NI CHELSEA TU NDIO IMEBAKI KWENYE MBIO ZA UBINGWA” WENGER ADAI

on

BAADA ya Chelsea kushinda mechi 12 mfululizo kabla ya mechi ya Jumamosi,
kocha wa Arsenal, Arsene Wenger fasta amedai: “Timu moja tu Chelsea ndio
imebaki kwenye mbio za ubingwa.”
Wenger haoni uwezekano wowote wa Liverpool, Man City, Man United, Tottenham
wala timu yake kutwaa taji msimu huu isipokuwa timu hiyo ya darajani.
Hata hivyo, bosi wa Chelsea, Antonio Conte anakosoa utabiri wa Wenger na
kudai kwamba Ligi ndio kwanza mbichi na ubingwa hauko mikononi mwao.
“Nadhani ni vigumu sana kujibu swali hili. Tumecheza mechi 18 bado kuna
mechi nyingine 20 kumalizia msimu huu.”
Mwanzoni mwa msimu huusio kocha, mwandishi wa habari wala mtu yeyote
aliyetegemea Chelsea ingekuwa miongoni mwa timu zinazotajwa kutwaa ubingwa na
hiyo ni kutokana na msimu mbaya uliotangulia.
“Hatukufanya vizuri kwenye soko la wachezaji lakini sasa nimefurahi kuona
mambo yamebadilika. Nina shaka kidogo ninapopata mabadiliko mazuri haraka
haraka kiasi hiki. Hii inanifanya niwe makini.”
“Tuko mbele kwa pointi sita tu dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili na
pointi saba timu katika nafasi ya tatu.”
“Nadhani safari ni ndefu, nimefurahishwa na jinsi wachezaji wangu
wanavyopitia mabadiliko mazuri.”

“Jambo la muhimu kwetu ni kuhakikisha tunapigana kwa nguvu zaidi, akili
yetu iwe kwenye soka kushinda mechi 12 hazitoshi kusema sisi tayari mabingwa
msimu huu.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *