NICKI MINAJ, NEEK MILL WATUPIANA VIRAGO… vijembe vyaanza kutawala kati yao

RAPA Nicki Minaj na Neek Mill wameachana.

Minaj, 34, aliandika ujumbe wa Twitter Alhamisi: “Nathibitisha ndio niko singo, naweka akili kwenye kazi yangu na najiandaa kushea nanyi hivi karibuni, muwe na mwaka mpya wenye baraka, nawapenda.”

Uvumi wa wawili hao kuachana ulitawala Internet mwezi uliopita baada ya rapa huyo mwenye umri wa miaka 29 kufuta akaunti yake ya Instagramu na huku kimwana huyo akiandika meseji za mafumbo kudokeza mahusiano yao yaliyovunjika.

Minaj aliposti ujumbe uliosomeka: “Thamani yako haishuki kwa kuwa tu mtu hana uwezo wa kuiona thamani yako.”

Pia akaposti picha ya makubadhi na mashairi ya wimbo wa Beyonce: “Best thing never had” iliyotafsiriwa kuwa ni dongo kwa mwanaume huyo akimaanisha kwamba makubadhi ndio kitu bora zaidi alichopata kuwa nacho maishani mwake.


Wawili hao walithibitisha kuwa wapenzi mwezi Machi, 2015.

No comments