NISHA ASEMA "SKENDO" ZA MWAKA 2016 ZILIKUWA NI ZA KIBIASHARA TU... awataka mashabiki wake kuzipotezea

NYOTA wa Bongomuvi, Salma Jabu “Nisha” amewataka mashabiki wake wa filamu kuachana na “skendo” zote alizopitia mwaka 2016 kwa madai kwamba ni “kiki” za kibiashara.

Msanii huyo alisema kuwa mwaka 2016 alitoa filamu moja ya “Kiboko Kabisa” huku akitumia muda mwingi kwenye biashara zake na sasa amerudi upya kwenye Bongomuvi ili kuendelea kuwapa uhondo mashabiki wake.

Alisema, mwaka huu ni wa kuziba pengo la filamu akiwa na kampuni yake ya Nisha’s Film Production kwa vile ameshaweka sawa biashara zake za vipodozi na nguo.

“Mwaka 2016 ulikuwa ni wangu wa kufanya biashara tofauti na filamu na nimefanya biashara kwa lengo la kuweka misingi imara ya kujiingizia kipato bila kutumia filamu,” alisema Nisha.

Mwishoni mwa mwaka jana msanii huyo alidai kubakwa na kupachikwa ujauzito, jambo ambalo baadae alisema halikuwa la kweli bali ni “kiki” tu.
  

No comments