NYOTA WA BOLLYWOOD ALIYEANGUKA AKIIGIZA APATA NAFUU NA KUANZA KUZUNGUMZA


MWIGIZAJI nyota wa India, Priyanka Chopra, 34, amezungumza na mashabiki wake kwa mara ya kwanza tangu alipojeruhiwa baada ya kuangukia kichwa wakati akiigiza Alhamisi iliyopita.

Kimwana huyo amewashukuru mashabiki wake katika ujumbe wa Twitter akisema; “Asanten kwa dua zenu.”

Kwa mujibu wa TMZ mwigizaji huyo aliteleza na kuangukia kichwa wakati akiigiza.

Mwakilishi wake alisema; "Chopla aliwahishwa hospitali haraka akafanyiwa uchunguzi na madaktali na kuruhusiwa kwa sasa anaendelea na ushauri wa madaktari."

No comments