NYOTA WA ZAMANI WA MLIMANI PARK SIKINDE AUTETEA MUZIKI WA DANSI… asema haujafa na wanaodai umeshuka wana maslahi na mitindo mingine

MKALI wa nyimbo “Maluma” na “Asha Bora” za Mlimani Park Sikinde, Julius Mzeru ambaye kwa sasa anamiliki timu yake binafsi ya “Mbeta Band”, ameutetea muziki wa dansi akisema bado uko kwenye chati.

Akiongea na Saluti5, Mzeru amesema kuwa hakubaliani na mawazo ya baadhi ya wadau na mashabiki kuwa muziki wa dansi umepoteza msisimko, ambapo anadai kuna kundi la watu wanaolazimisha muziki huo upotee kwa maslahi yao binafsi.

“Dansi bado liko katika ubora wake na aina nyingine zote za muziki zitakuja na kupita na kuliacha linapeta, dhana ya kwamba muziki huo umeshuka zinasababishwa na baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi,” amesema.


Mzeru ambaye enzi zake akiwa Sikinde alitunga vibao “Asha Bora” na “Maluma”, anasemekana ndie mpigaji gitaa la besi aliyerekodi nyimbo nyingi zaidi katika bendi hiyo.

No comments