OGOPA KOPAZ SASA KUSHUSHA MAJINZI, MADILA YENYE NEMBO YA BENDI YAO

BAADA ya kuchapisha Tisheti zenye nembo ya bendi yao, Ogopa Kopaz Classic Band sasa wanakuja na nguo nyingine mbalimbali yakiwemo majinzi na madila ambayo vilevile nayoyatakuwa na nembo ya bendi hiyo.

Bosi wa Ogopa Kopaz, Malkia Khadija Omar Kopa aliiambia Saluti5 kuwa lengo lao ni kuwatafutia wasanii wao njai rahisi ya kujikimu nje ya bendi kwa kuwaingiza pia kwenye ujasiriamali.


“Tumekusudia kuanzisha miradi mbalimbali yakiwemo maduka ya Ogopa Kopaz ambazo yatakuwa yakiuza bidhaa zetu mbalimbali zikiwemo CD, Tisheti, majinzi na madila yenye nembo ya bendi,” amesema Kopa.

No comments