KIUNGO wa bei mbaya wa Manchester United Paul Pogba amesema makali yake anayoyaonyesha hivi sasa yanatokana na ushauri wa kocha Jose Mourinho.

Pobga mwenye umri wa miaka 23, aliyerejea Manchester United msimu huu kutoka Juventus kwa usajili wa rekodi ya dunia, alikuwa na mwanzo mbaya lakini sasa ameanza kutakata na kuonyesha ubora wake.

Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania, amesema Mourinho alimpa moyo na kuwambia ajiachie uwanjani na kucheza vile atakavyo.

"Mourinho aliniambia nisimsikilize mtu yeyote, niweke akili yangu dimbani na kufurahia soka langu na hicho ndicho ninachofanya," Pobga aliiambia BBC.

"Alizungumza na mimi. Alinifanya nijisikie amani na mwenye kujiamini. Aliniambia 'unajua namna ya kucheza, fanya kile utakacho'. Alininitaka niwe huru uwanjani. Hicho ndicho nilichotaka kusikia kutoka kwa kocha wangu".

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac