PAUL SCHOLES ASEMA MESSI NI MCHEZAJI WA KIWANGO CHA JUU KUMZIDI RONALDO

HUU ni mtazamo wa Paul Scholes anayetathmini kuwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi ni mchezaji wa kiwango cha juu kumzidi winga wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ambaye sasa anakipiga Real Madrid.

Schools akinukuliwa amesema kwa mtazamo wake ni kwamba Messi ni mchezaji bora wa miaka kumi ya hivi karibuni wa dunia.

Akiandika kutoka makala binafsi, Scholes alisema:
“Nafikiri kuhusu aina ya wachezaji wakubwa niliowahi kucheza nao dimbani, Eric Cantona, Zinedine Zidane, Pirlo Xabi na Cristiano Ronaldo, lakini katika orodha hiyo yote Lionel Messi ni mchezaji mkubwa na bora kuliko wote hao. 

Huu ni mtazamo wangu ambao naamini ni sahihi.”

Schools mwenye umri wa miaka 40, sasa aliyazungumza hayo akiamini Mess indie mchezaji wa kuchungwa kwa sasa kwa timu yoyote inayocheza na Barcelona ama dhidi yake.

No comments